RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV LIVE

PROPHET TB JOSHUA INVITED RULEA SANGA FROM TANZANIA TO SEE HIM -SCOAN NIGERIAL APRIL 2012

T.B. JOSHUA EMPOWERS SCOAN LONDON 1ST SEPTEMBER 2013 SERVICE!

Thursday, July 5, 2012

ANNOITING WATER YAMSHANGAZA-SOFIA

 NabiiTB Joshua
Dada Sofia ni mjasiliamali ambaye anayejishughulisha na biashara ya nguo maeneo ya Sinza kwa Remy kama unaelekea Kanisa la Katoliki.

Anasema, siku moja alikutana na blogger Rulea Sanga na kumuomba atumie maji ya upako kutoka kwa Nabii TB Joshua wa Nigeria. Baada ya kupewa alikunywa na akamgawia House Girl wake na mtoto wake ambaye ni mdogo sana.  Mtoto alipopewa mafuta hayo alianguka chini na kuwa kimia kwa muda kidogo, kitendo hicho kilimchanganya sana dada Sofia na kuhangaika kuntafuta Rulea Sanga ili amuulize nini kinaendelea kwa mtoto, alikuwa na hofu sana kuwa mume wake akisikia utakuwa ni ugomvi.

Baada ya muda si mrefu yule mtoto aliamuka na kucheza kama kawaida yake akiwa na furaha sana. Sofia alimchukua yule mtoto na kumpeleka kwa mchungaji wake ili kujua zaidi. Mchungaji baada ya kupokea habari hizo alimuombea na baadae kugundulika kuwa alikuwa na mapepo. Huyo mtoto anaendelea vizuri na hana tatizo lolote.

Mbali na muujiza wa mtoto, dada sofia amesema tangia amemwagia yale maji katika biashara yake, amekuwa anapata wateja wengi sana, na hata wale waliokuwa anawadai na walikuwa wanamsumbua, wamekuwa wakimpigia simu na kurudisha madeni yao. Sofia anamshukuru sana Mungu kwa wema wako na alimshukuru sana Rulea Sanga aliyempa hayo maji ya upako.

Sofia amnasema ni mengi ameyapata mbali na Annoiting Water. Emmanuel Tv ni Tv ambayo inamilikiwa na kanisa la TB Joshua. Sofia nyumbani muda mwingi anakuwa katika TV hiyo akishirikiana na maombezi yanayoendelea huko Nigeria. Kwa kupitia TV hiyo amefanikiwa sana kibiashara. Wateja wamekuwa ni wengi na wale waliokuwa wanadaiwa wamekuwa wakirudisha madeni wenyewe kwa kumtafuata.

Hiyo ndiyo miujiza aliyopata dada yetu


No comments:

Post a Comment