RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV LIVE

PROPHET TB JOSHUA INVITED RULEA SANGA FROM TANZANIA TO SEE HIM -SCOAN NIGERIAL APRIL 2012

T.B. JOSHUA EMPOWERS SCOAN LONDON 1ST SEPTEMBER 2013 SERVICE!

Sunday, June 10, 2012

RULEA SANGA APONYWA SHINGO BAADA YA KUTUMIA “ANOITING WATER”  YA 
NABII TB JOSHUA SIKU YA JUMAMOSI


Rulea Sanga
Usiku wa jumamosi nilikuwa naumwa sana na shingoni wakati wa kumeza chakula au kinywaji,  hali hii  ilinisababishia kupata malaria, ilikuwa hali mbaya sana. Nilikuwa nashindwa kumeza chakula au kinywaji chochote kutokana na maumivu makali shingoni. Muda ulivyokuwa unaenda ndivyo maumivu yalikuwa yanazidi. Hali hii ilinikosesha rah asana, sikupenda hata kuongea kwa mwili wangu ulidhoofika sana.

Nabii TB Joshua
Rosemary aliponipigia simu, alishangazwa sana na maongezi yangu kuwa si ya kawaida kutoka na kushindwa kuongea vizuri, na aliponiuliza nilimjibu kuwa naumwa sana. Alinifariji sana na kuniambia nisitumie tena maji ya moto na nimeze panadol kwaajili ya kuondoa maumivu. Nilimshukuru sana kwa kunitia moyo na kunisaidia kimawazo, lakini nilimwambia sina panadol na ni usiku siweze kupata duka la dawa, bali nilichomwambia ni kwamba usiku wa leo ninaenda kupona kwa jina la Yesu Kristo.

Niliondoka na kuelekea chumbani kwangu na kuchukua yale maji ya upako ya TB Joshua na kuyanywa. Niliamini kwa kupitia maji haya naenda kupona. Muda ulipofika wa kwenda kulala nikahisi maumivu kama yanapungua. Asubuhi nilipoamka maumivu yote yalitoweka na nikawa na uwezo wa kunywa na kula. Nikamtuma kijana wangu Alex kwenda kununua mihogo ili nione kama naweza kumeza huku nikishushia na Coca Cola ya baridi…..Mihogo ilipita bila kikwazo chochote.

Ninamshukuru sana Mungu wangu kwa uponyaji, na ninamshukuru sana Nabii TB Joshua kwa kupitia “Anoiting Water”

Kumbuka mwezi April niliitwa na Nabii TB Joshua na kunikabidhi maji haya ya upako

Bonyeza hapa kuona nilivyokuwa SCOAN Nigeria kwa Nabii TB Joshua:
http://rumaafrica.blogspot.com/p/tb-joshua-invited-rulea-sanga-and.html

Mungu ni mwema kwangu daima.

Wenu

Rulea Sanga

No comments:

Post a Comment